Mapigano kati ya askari wa India na Pakistan katika eneo la
mpakani la Kashmir kwa siku mbili mfululizo, yamepelekea makumi ya
maelfu ya wanavijiji wa eneo hilo kukimbia makazi yao. Raia wasiopungua
10 wameripotiwa kuuawa na wengine 22 kujeruhiwa katika utupianaji risasi
na makombora kati ya askari polisi wa India na wa eneo la Pakistan la
Kashamir.
Shams Uddin afisa polisi wa Pakistan amesema kuwa eneo
zima la vijiji na milima kwenye mpaka limeathiriwa na mapigano hayo,
huku maelfu ya watu wakikimbia nyumba zao kuelekea kwenye maeneo salama.
Machafuko hayo yanahesabiwa kuwa ni ukiukwaji mbaya zaidi
wa makubaliano ya usitishaji vita yaliyofikiwa mwaka 2003 kati ya India
na Pakistan.

Facebook
Twitter
RSS
0 toamaon yako: