Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Wednesday, October 8

Kundi la Ansarullah lapinga uteuzi wa waziri mkuu mpya wa Yemen

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Kundi la Ansarullah lapinga uteuzi wa waziri mkuu mpya wa YemenBaada ya kufikiwa makubaliano kati ya serikali na vyama vya kisiasa vya Yemen kuhusu kuundwa serikali mpya, Rais Abd Rabbuh Mansur Hadi wa nchi hiyo amempa jukumu la kuunda serikali Ahmed Awadh bin Mubarak aliyekuwa mkuu wa ofisi ya rais. Lakini hivi sasa uteuzi huo umekumbwa na utata. Hii ni kwa sababu harakati ya Ansarullah na chama cha Kongresi ya Taifa ya Ukombozi wa Yemen vimepinga kuchaguliwa uteuzi huo. Kabla ya makubaliano hayo ilikubaliwa kuwa, uteuzi wa waziri mkuu mpya ufanyike kwa maafikiano ya vyama vyote na makundi ya kisiasa ya Yemen. Ingawa makamu wa rais wa Yemen ametangaza kuwa uteuzi wa Mubarak kama waziri mkuu mpya umefanyika baada ya maafikiano ya vyama vyote, lakini ushahidi uliopo ni kinyume na madai hayo. Wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa wanaamini kuwa, iwapo harakati ya Ansarullah itaendelea kupinga kuteuliwa bin Mubarak kuwa waziri mkuu, suala hilo linaweza kuandaa mazingira ya kuibuka mgogoro mpya nchini Yemen. Hasa kwa kuzingatia kuwa, pande mbili za mgogoro wa Yemen ambazo ni serikali na harakati ya Ansarullah bado haziaminiani. Suala hilo linadhihirishwa wazi na msimamo uliochukuliwa hivi karibuni wa harakati ya Answarullah. Harakati hiyo inasema kuwa, uteuzi wa Bw. Ahmad Awadh bin Mubarak aliyepewa jukumu la kuunda serikali mpya ya Yemen umefanyika baada ya kufanyika mazungumzo baina ya balozi wa Marekani na Rais Abdu Rabuh Mansur Hadi. Hii inaamanisha kuwa, viongozi wa Washington wana nafasi katika kuainisha waziri mkuu mpya wa Yemen. Harakati ya Ansarullah imetangaza rasmi kuwa, uteuzi wa bin Mubarak haukufanywa ndani ya nchi. Kwa ajili hiyo kundi hilo halitaki kwa mara nyingine Abdu Rabah Mansur Hadi ampe jukumu la kuunda Baraza la Mawaziri mtu ambaye amechaguliwa na Wamagharibi. Hivi karibuni hali ya Yemen ilikuwa ni ya kimapinduzi. Wananchi wa nchi hiyo walijitokeza mabarabarani na kupiga nara za kutaka Rais Abd Rabbuh Mansur Hadi aondoke madarakani na serikali yake ibadilishwe. Mwishowe kutokana na mashinizo ya walio wengi na kwa mujibu wa makubaliano yaliyofikiwa chini ya upatanishi Umoja wa Mataifa kati ya Ansaruddin na serikali ya Sana'a, Abdu Rabbuh alikubali kubadilisha serikali. Walikubaliana kuwa serikali mpya iundwe na waziri mkuu atakayeafikiwa na vyama vyote vya kisiasa. Lakini kwa kuwa hakuna kuaminiana kati ya pande hizo mbili, kuna swali linalojitokeza hapa kwamba, je, makundi ya Yemen yanaweza kumuarifisha waziri mkuu atayakayekubaliwa na pande zote? Hapana shaka kuwa suala hilo linaweza kufanikiwa iwapo mitazamo ya vyama vyenye taathira na viongozi wanaotawala Yemen kuhusu kuundwa serikali itakakaribiana. Kwa kuzingatia kuwa Marekani inataka kuwa na nafasi kubwa zaidi katika maamuzi ya Yemen, je, kuna matumaini ya kuundwa serikali ya kitaifa itakayoafikiwa na makundi yote nchini humo? Kwa kuzingatia kuwa mtazamo wa serikali ya Sana'a na harakati ya Answarullah kuhusiana na Wamagharibi unatofautiana, ni wazi kuwa, suala hilo ni jambo gumu kwa Yemen. Iwapo pande za nchi hiyo hazitoafikiana haraka kuhusu nafasi ya waziri mkuu, kuna uwezekano matukio mapya yakashuhudiwa nchini Yemen, ambapo kuvunjwa makubaliano ya usitishaji vita ni matokeo mabaya zaidi ya suala hilo.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com