
Bi Marzie Afkham amesema hayo leo Jumatano mbele ya waandishi wa habari na kuongeza kuwa, ripoti ya Ahmed Shaheed, mjumbe maalumu wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusiana na Iran imeangalia mambo kwa upande mmoja na hayana ukweli wowote. Ameongeza kuwa, Ahmed Shaheed kimsingi amekuwa mwendesha siasa zilizo dhidi ya Iran.
Amma kuhusiana na duru ijayo ya mazungumzo ya nyuklia na kundi la 5+1 Bi. Afkham amesema, mazungunzo ya pande mbili na pande kadhaa baina ya Iran na kundi hilo yataendelea wiki ijayo huko Vienna, Uswisi.
0 toamaon yako: