
Spika wa Majilisi ya Ushauri ya Kiislamu
(Bunge la Iran) amesema kuwa umoja na mshikamano kati ya makundi ya
kisiasa nchini Iraq ndio unaoweza kukomesha misimamo mikali na machafuko
katika nchi hiyo ya Kiarabu. Ali Larijani amesema hayo leo wakati
alipoonana na Waziri wa Vijana na Michezo wa Iraq Abdul Huddein Abrani
hapa mjini Tehran na kuongeza kuwa, umoja wa kitaifa na mshikamano kati
ya makundi ya kisiasa ya Iraq unao uwezo wa kuzuia kuenea machafuko na
makundi yenye misimamo mikali nchini Iraq. Kiongozi huyo wa juu kabisa
katika Bunge la Iran ameongeza kuwa, ana matumaini kuundwa serikali mpya
Iraq kutafungua njia ya kudumishwa amani na kupambana vilivyo na
makundi ya kigaidi nchini humo. Amesema, uongozi mzuri wa wanasiasa
nchini Iraq na kuundwa serikali mpya nchini humo kunaweza kupunguza
matatizo waliyo nayo wananchi wa Iraq hivi sasa. Kwa upande w
ake Bw.
Abdul Hussein Abtan, Waziri wa Vijana na Michezo wa Iraq ameishukuru
serikali na wananchi wa Iran kwa uungaji mkono wao kwa taifa la Iraq na
kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima imekuwa muungaji mkono
wa mapambano dhidi ya ugaidi na kudumishwa amani na utulivu nchini Iraq
na kwamba wananchi wa Iraq kamwe hawawezi kusahau msaada huo wa wananchi
na serikali ya Iran kwao.
0 toamaon yako: