Mbunge Msuni katika Majlisi ya Ushauri
ya Kiislamu (Bunge la Iran) amesema kuwa, Waislamu wa Kisuni nchini Iran
wanalichukia kundi la kigaidi la Daesh. Bw. Muhammad Qasim Uthmani,
mmoja wa wabunge hao amesema leo katika kikao cha wazi cha Bunge la Iran
kwamba Masuni wa Iran wanalaani vikali jinai za kundi la kigaidi na
kibaath la Daesh nchini Iraq na Syria na kuongeza kuwa, baada ya j
inai
zilizofanyika huko Ghaza Palestina na Shangal nchini Iraq, sasa ni
wakati wa kufanyika jinai katika eneo la Kobani huko Syria. Mbunge huyo
wa Iran ameongeza kuwa, mji wa Kobani na wananchi wasio na ulinzi wa mji
huo wananyanyaswa na kuuliwa kinyama hivi sasa na kundi lenye fikra
potofu la Daesh. Bw. Uthmani ameongeza kuwa, inasikitisha kuona kuwa,
kama ilivyo mara zote, jamii ya kimataifa imekaa kimya kuhusiana na
jinai hizo kwani jamii hiyo imedhibitiwa na Marekani. Mbunge huyo Msuni
katika Bunge la Iran ameongeza kwamba: Kundi la Daesh ambalo limeundwa
na Marekani, limefanya mauaji na jinai kubwa dhidi ya wananchi wa Syria
lakini Marekani hiyo hiyo inajitokeza hadharani na kuthubutu kusema kuwa
inaunga mkono haki za binadamu. Mbunge huo ameashiria uungaji mkono wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa wananchi Wakurdi wa Iraq na kuongeza
kwamba serikali ya Uturuki si tu kwamba haiwasaidii wananchi Wakurdi wa
Kobani huko Syria, bali hata inazuia kuwafikia misaada ya kibinadamu
wananchi hao.


Facebook
Twitter
RSS
0 toamaon yako: