
Serikali ya Australia imepiga marufuku
kuingia nchini humo wahubiri wa dini ya Kiislamu wenye misimamo ya
kufurutu mipaka. Tony Abbott Waziri Mkuu wa Australia amesema kuwa,
ofisi za ubalozi za nchi hiyo zimepewa jukumu la kuhakikisha wanadhibiti
utoaji viza kwa wahubiri wenye misimamo mikali kuingia nchini humo.
Abbott amesisitiza kwamba, hakuna haja kwa sheria hiyo kupitishwa
bungeni. Msimamo wa serikali ya Australia umechukuliwa baada ya mhubiri
mmoja kutoka kundi la Hizbul Tahrir kutoa matamshi makali wiki iliyopita
mjini Sydney kwamba, wanataka kuweka dola la Kiislamu nchini humo.
Waziri Mkuu wa Australia ameongeza kuwa, hatua ya kupiga marufuku
kuingia nchini humo wahubiri wenye m
isimamo mikali ina lengo la kuzuia
kujitokeza uadui, chuki na mifarakano kati ya wananchi wa nchi hiyo.
0 toamaon yako: