
Uhuru Kenyatta leo amehudhuria kikao
maalumu cha Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC iliyoko nchini Uholanzi,
kwa lengo kujibu tuhuma zinazomkabili za kuhusika kwenye machafuko
yaliyotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya. Kwenye
vikao vilivyofanyika mahakamani, Kenyatta ameonekana akiwa makini
kumsikiliza mwendesha mashtaka wa ICC na wakati mwingine alionekana kuwa
ni mwenye mfadhaiko. Mwendesha Mashtaka wa ICC amesema kuwa, Kenyatta
hakutoa ushirikiano wa kutosha kwa mahakama hiyo wakati wa kufuatilia
rekodi zake za ulipaji kodi,rekodi za simu na taarifa za kibenki.
Kenyatta amesema kuwa, mashtaka yaliyofunguliwa dhidi yake ni ya kisiasa
na kusisi
tiza kwamba kesi hiyo inapaswa kufutwa. Uhuru Kenyatta ambaye
aliamua kutangaza kujiengua kwenye wadhifa wake wa urais kwa shabaha ya
kushiriki kwenye vikao vya mahakama ya ICC, anakabiliwa na mashtaka
matano yaliyosababisha kuibuka machafuko na ghasia zilizotokea baada ya
uchaguzi mkuu wa mwaka 2007, na kusababisha watu 1,200 kuuawa na wengine
600,000 kuyahama makazi yao.
0 toamaon yako: