Leo ni Jumatano tarehe 13 Dhilhaji 1435 Hijria sawa na tarehe 8 Oktoba 2014.

Siku kama ya leo miaka 24
iliyopita, kwa mara nyingine tena utawala haramu wa Israel ulifanya
jinai nyingine ya kinyama kwa kuwashambulia waumini wa Kipalestina
waliokuwa wakisali ndani ya Msikiti mtukufu wa al-Aqsa huko Palestina
inayokaliwa kwa mabavu. Wapalestina 20 waliuawa shahidi na makumi ya
wengine kujeruhiwa. Mauaji ya Wapalestina yaliyofanywa na utawala
ghasibu wa Israel tena ndani ya Msikiti wa al-Aqsa, kwa mara nyingine
tena yalilipua ghadhabu za walimwengu dhidi ya utawala huo katili. Hata
hivyo kama kawaida, uungaji mkono wa Marekani kwa Israel ulizuia
kuchukuliwa hatua yoyote ya kivitendo dhidi ya utawala huo.
Na miaka 9 iliyopita katika
siku kama ya leo, mtetemeko mkubwa wa ardhi uliokuwa na ukubwa wa 7.8
kwa kipimo cha Rishta uliyakumba maeneo ya kaskazini mashariki mwa
Pakistan. Kitovu cha mtetemeko huo kilikuwa katika mji wa Muzaffarabad.
Watu karibu 90,000 walipoteza maisha yao na wengine 3,300,000 kubaki
bila makazi.
0 toamaon yako: