Leo ni Jumanne tarehe 12 Dhilhaji 1435 Hijria sawa na Oktoba 7, 2014.
Siku kama ya leo miaka 13
iliyopita sawa na tarehe 7 Oktoba 2001, Marekani iliivamia Afghanistan.
Uvamizi huo ulifanyika kwa kisingizio cha kuliangamiza kundi la
wanamgambo wa Al-Qaida ambao kwa mujibu wa Washington walihusika na
tukio la Septemba 11 2001 nchini Marekani. Katika kip
indi cha wiki
kadhaa, ndege za kivita za Marekani, zilifanya mashambulizi dhidi ya
ngome za kundi la Taliban ambalo katika kipindi hicho lilikuwa
likidhibiti eneo kubwa la ardhi ya Afghanistan sambamba na kuliunga
mkono kundi la Al-Qaida lililokuwa likiongozwa na Osama bin Laden.
Mashambulizi hayo mazito ya Marekani yaliua na kujeruhi maelfu ya raia
wasio na hatia wa Afghanistan huku wengine wakilazimika kuwa wakimbizi.
Hata hivyo pamoja na Marekani kusaidiwa na muungano wa vikosi vya
kaskazini mwa Afghanistan na kufanikiwa kuuangusha utawala wa Taliban,
hadi leo haijaweza kumtia mbaroni Mulla Omar na viongozi wengine wa
kundi hilo la Taliban.
Miaka 65 iliyopita, Ujerumani
ya Mashariki iliasisiwa na kuwa na mfumo wa Jamhuri ya Kidemokrasia.
Katika miezi ya mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia, Shirikisho la
Umoja wa Sovieti liivamia na kuikalia kwa mabavu ardhi ya Ujerumani ya
Mashariki, na madola ya Magharibi yakadhibiti sehemu ya magharibi mwa
nchi hiyo. Hata hivyo baadaye Umoja wa Sovieti ulijitoa katika Baraza la
Makamanda wa Waitifaki baada ya kutofautiana na madola ya Magharibi juu
ya namna ya kuiendesha nchi hiyo.
Na siku kama ya leo miaka 74
iliyopita, yaani tarehe saba Oktoba mwaka 1940 majeshi ya Ujerumani ya
Kinazi yaliidhibiti na kuikalia kwa mabavu ardhi ya Romania katika
kipindi cha Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Kwa utaratibu huo, uwanja wa
majeshi ya Ujerumani wa kuishambulia ardhi ya lililokuwa Shirikisho la
Umoja wa Sovieti mnamo Juni 1941 ukawa umeandaliwa.

Facebook
Twitter
RSS
0 toamaon yako: