Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Wednesday, October 8

Jumapili, 05 Oktoba, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Jumapili, 05 Oktoba, 2014Leo ni Jumapili tarehe 10 Dhul-Hijja mwaka 1435 Hijria, sawa na tarehe 5 Oktoba mwaka 2014 Miladia.
Leo tarehe 10 Dhilhaj ni sikukuu ya Idul Adh'ha, moja ya sikukuu kubwa za Kiislamu. Katika siku hii mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu waliokwenda Makka, huchinja mnyama kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mola wao na kuhuisha kumbukumbu ya Nabii Mtukufu Ibrahim (as). Mwenyezi Mungu aliijaribu imani na ikhlasi ya Nabii huyo kwa kumuamuru amchinje mwanawe kipenzi Ismail (as). Licha ya mashaka ya utekelezwaji wa amri hiyo, Nabii Ibrahimu (as) aliandaa mazingira ya utekelezwaji wake na kumlaza chini mwanaye huyo na kuanza kuikata shingo yake lakini kisu kilikataa kuchinja. Hapo ndipo akaambiwa na Mwenyezi Mungu kuwa amefaulu mtihani huo na akamtumia mnyama wa kuchinja badala ya mwanaye Ismail. Tukio hili lenye ibra na mafunzo tele linawapa wanadamu somo la kujitoa mhanga, kujisabilia kwa ajili ya Allah, kushinda matamanio na matakwa ya nafsi na kusalimu amri mbele ya amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Redio Tehran inatoa mkono wa baraka na fanaka kwa Waislamu kote duniani kwa mnasaba wa sikukuu hii kubwa.
Siku kama ya leo miaka 36 iliyopita, Imam Khomeini (MA) Mwasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran alihama Iraq na kuelekea Paris Ufaransa. Imam Khomeini aliamua kufanya hijra hiyo ya kihistoria wakati utawala wa zamani wa Iraq ulipoanza kumzuia ache harakati zake za mapambano dhidi ya utawala wa Shah. Serikali ya wakati huo ya Iraq ambayo ilikuwa ikilinda mahusiano na utawala wa Shah nchini Iran, ilimtaka Imam Khomeini ajiepushe na harakati zozote za kisiasa na za kimapinduzi dhidi ya utawala huo wa Shah. Hata hivyo Imam aliimbia serikali hiyo kuwa hilo lilikuwa ni jukumu lake la kisheria ambalo aliwajibika kulitekeleza na kusisitiza juu ya kuendeleza mapambano yake kwa kutoa hotuba na kutuma kanda za kimapinduzi nchini Iran.
Siku kama ya leo miaka 14 iliyopita, Slobodan Milosevic dikteta wa Yugoslavia na muhusika mkuu wa vita vya umwagaji damu huko Balkan, alijiuzulu baada ya miezi kadhaa ya malalamiko ya ndani na vikwazo vya kimataifa. Milosevic alikuwa rais wa Serbia tangu mwaka 1990 hadi 1997 na baadaye akawa rais wa Jamhuri ya Yugoslavia. Katika vita vya Bosnia, na kwa uungaji mkono wa kila upande wa Waserbia, Slobodan Milosevic alishiriki pakubwa katika kutekeleza mauaji ya kizazi dhidi ya Waislamu wa Bosnia. Slobodan Milosevic alikuwa kiongozi wa kwanza mtenda jinai za kivita kuwahi kufikishwa katika mahakama ya kimataifa kwa ajili ya kuhukumiwa.
Na siku kama ya leo miaka 150 iliyopita, alizaliwa Louis Jean Lumiere, mwanakemia mwanaviwanda mashuhuri wa Kifaransa. Mwaka 1895 akiwa pamoja na ndugu yake, aliyejulikana kwa jina la Auguste Lumiere, walifanikiwa kutengeneza kifaa ambacho kiliwasaidia kuchukua picha mbalimbali na kusajili harakati. Mwaka huo huo Lumiere alifanikiwa kuonyesha filamu yake ya kwanza au Motion Picture katika majumba ya sinema.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com