Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Wednesday, October 8

Jumamosi, Oktoba 4, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Leo ni Jumamosi tarehe  9 Mfunguo Tatu Dhil-Hija mwaka 1435 Hijria mwafaka na tarehe 4 Oktoba mwaka 2014 Miladia.
Jumamosi, Oktoba 4, 2014Leo ni siku ya Arafa tarehe 9 Dhil-Hija. Arafa ni jina la jangwa kubwa linalopakana na mlima wa Jabalur Rahma ulioko kusini mashariki mwa Makka. Tangu adhuhuri ya siku hii mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu al Kaaba husimama katika uwanja wa Arafa na hadithi nyingine za Kiislamu zimetaja fadhila na utukufu mkubwa wa kisimamo hicho. Hadithi zinasema kuwa Mwenyezi Mungu SW ameifa nya ardhi ya Arafa ambayo ilikuwa medani ya matukio mengi muhimu ya kihistoria, kuwa mahala pa kuwapokea wageni wake wanaokwenda Hija na ameweka meza na karamu yake pembeni ya mlima wa Jabalur Rahma. Ni vyema kukumbusha kuwa magharibi ya siku hii ya leo mahujaji wanaondoka uwanja wa Arafa na kuelekea Mash'arul Haram na kujitayarisha kwa ajili na amali nyingine za Hija. ***
Siku kama ya leo miaka 1375 iliyopita, Muslim bin Aqil binamu wa Imam Hussein bin Ali bin Abi Talib AS aliuawa shahidi mjini Kufa Iraq. Alikuwa mmoja wa shakhsia wakubwa na wacha Mungu katika zama zake. Alielekea mjini al-Kufa, Iraq akiwa na lengo la kwenda kutathmini ni kwa kiwango gani watu wa mji huo walikuwa wakimtii Imam Hussen, baada ya watu wa mji huo kumwandikia maelfu ya barua Imam huyo wakimtaka aende mjini humo na kwamba wako tayari kumuunga mkono katika harakati yake dhidi utawala dhalimu wa  Yazid bin Muawiya. Watu wa Kufa walimsaliti Muslim bin Aqil baada ya kuhadaika kwa hila na uongo wa Ubeidullah bin Ziyad, mtawala wa wakati huo wa Kufa na wakamuacha Muslim bin Aqiil peke yake. ***
Siku kama ya leo miaka 48 iliyopita nchi ya Kiafrika ya Lesotho ilipata uhuru kutoka kwa mkoloni Muingereza. Kabla ya uhuru, Lesotho ilikuwa ikijulikana kwa jina la Basutoland na kuanzia mwaka 1884 ikawa chini ya mkoloni Mwingereza. Uingereza iliendelea kuikalia kwa mabavu Lesotho hadi mwaka 1966 na hatimaye nchi hiyo ikapata uhuru kamili katika siku kama ya leo. Lesotho iko kusini mwa bara la Afrika huku ikiwa imezingirwa na jirani yake Afrika Kusini. ***
Miaka 57 iliyopita katika siku kama ya leo satalaiti ya kwanza ilirushwa angani na msomi wa Urusi ya zamani na kwa utaratibu huo zama za udhibiti wa anga zikaanza. Satalaiti hiyo iliyopewa jina la Sputnik 1 ilizunguka dunia mara 1400 kwa siku 92 na kwa mara ya kwanza ikafikisha ujumbe wa radio kutoka angani kuelekea ardhini. ***
Katika siku kama ya leo miaka 184 iliyopita  nchini ya Ubelgiji ilijitangazia uhuru wake. Kuanzia karne ya 18 Ubelgiji ilikuwa chini ya udhibiti wa Austria na mwishoni mwa karne hiyo hiyo ikawa chini ya udhibiti wa Ufaransa. Hata hivyo baada ya Napoleone Bonaparte kushindwa na madola ya Ulaya, mwaka 1815 Miladia, Ubelgiji na Uholanzi zilunda muungano. Hata hivyo muungano huo haukudumu baada ya Wakatoliki wa Ubelgiji kuanzisha uasi dhidi ya Waprotestani wa Uholanzi na kuitanga nchi yao kuwa huru. ***
Na tarehe 4 Oktoba mwaka 1963 yaani miaka 51 iliyopita kimbunga cheusi cha Caribbean kilianza na kuangamiza suhula zote za bandari na visiwa vya bahari ya Caribean. Kimbunga hicho angamizi kilikuwa na kasi ya kilomita 150 kwa saa na kwa ujumla kiliua karibu watu elfu sita wengi wao wakiwa raia wa Cuba na Haiti. *

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com