Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahamatullahi Wabarakaatuh. Karibuni wapenzi wasikilizaji katika sehemu hii nyingine ya mfululizo wa makala hizi fupi fupi zinazozungumzia amali zilizo bora. Ni makala ambazo zinakunukulieni "nusus" na hadith za maasumu kuhusu amali mbalimbali zilizo bora ambazo zinamkurubisha mno mja kwa Mola wake na kumletea manufaa ya duniani na Akhera. Miongoni mwa amali zilizo bora kabisa ni kujifunza Qur'ani na kuifundisha. Katika kitabu cha 'Iddatud Dai cha mwanachuoni mkubwa Ahmad bin Fahd al Hilli imepokewa hadith kutoka kwa Bwana Mtume Muhammad SAW akisema:
من أعطاه الله القرآن فرأى أن أحداً أعطي أفضل مما أعطي فقد صغّر عظيماً وعظّم صغيراً
Mtu ambaye amepewa Qur'ani na Mwenyezi Mungu akadhani kuna mtu mwingine amepewa kitu bora kuliko alichopewa yeye basi atakuwa amedunisha kitu adhimu na kutukuza kitu duni.
*******
Vile vile imepokewa hadithi katika kitabu hicho cha 'Uddatud Dai kutoka kwa Imam Sadiq AS akisema: Haimpasii muumini kufa kabla hajajifunza Qur'ani au kuwa katika kujifunza Qur'ani.
Na inawezekana siri ya kusisitiziwa vyote hivyo suala hilo ikawa imo katika hadithi zilizopokewa kutoka kwa Bwana Mtume Muhammad SAW katika kitabu cha Hadith cha al Wasail aliposema: Watu wa Qur'ani ni watu mahsusi wa Mwenyezi Mungu. Pia amesema: (أفضل العبادة قراءة القرآن) Ibada iliyo bora kabisa ni kusoma Qur'ani. Pia amesema: Qur'ani ni utajiri na hakuna utajiri bila ya Qur'ani na hakuna umaskini baada ya kumiliki Qur'ani.
Vile vile Sheikh Saduq amepokea hadithi katika kitabu cha Thawabul A'amaal kutoka kwa Imam Jaafar Sadiq AS akibainisha utukufu na baraka za Akhera za kushikamana na Qur'ani Tukufu kwa kusema: Mwenye kujibidiisha kusoma Qur'ani akiwa bado kijana, Qur'ani huchanganyika na nyama na damu yake na Mwenyezi Mungu humjaalia mtu huyo kuwa pamoja na wajumbe Wake watukufu walio wema yaani Malaika, na Qur'ani itakuwa hujja kwake Siku ya Kiyama hadi wa mwisho wa hadith.

Mwisho tunasoma katika kitabu cha Jaamiul Akhbar hadithi iliyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume Muhammad SAW akisema: Mwenye kumfunza mwanawe Qur'ani ni kama mtu aliyekwenda Hijja mara elfu kumi, akaenda Umra mara elfu kumi, akawaachilia huru watumwa elfu kumi kutoka kizazi cha Ismail AS, na akapigana vita elfu kumi katika njia ya Allah akawalisha Waislamu elfu kumi wenye njaa na ni kana kwamba amewavisha Waislamu elfu kumi wasio na nguo na Mwenyezi Mungu atamuandikia kwa kila herufi moja ya Qur'ani mema kumi na kumfutia kwa kila herufi moja maovu kumi na Qur'ani itaendelea kuwa naye hadi katika kaburi lake na atafufuliwa pamoja nayo na itaitia nguvu mizani yake na kumpitisha salama katika Sirat kwa kasi ya umeme na Qur'ani haitaachana naye hadi imfikishe kwenye mashukio bora kabisa anayoyatamani.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu atupe taufiki ya kushikamana vilivyo na Qur'ani Tukufu, kujifunza vizuri mafundisho yake na kuifundisha. Aamin.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.

Facebook
Twitter
RSS
0 toamaon yako: