Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

uislam 10 Amali Zilizo Bora

Posted by mkachu  |  Tagged as:


Amali Zilizo Bora (10)
Bismillahir Rahmanir Rahim. Assalaamu Alaykum Warahamatullahi Wabarakaatuh. Wapenzi wasikilizaji hii ni sehemu ya 10 ya mfululizo wa makala hizi fupi fupi za Amali Zilizo Bora. Leo makala yetu itatupia jicho baadhi ya hadithi za maasumu zinazobainisha fadhila za kuwapenda Ahlul Bayt AS na kuwatii. Zimepokewa hadithi sahihi zinazosema kuwa miongoni mwa amali zilizo bora kabisa ni kuwapenda Ahlul Bayt wa Mtume Muhammad SAW na kuwatii. Amali hiyo mbali na kuwa na ujira bora wa kimaanawi, ndilo jambo ambalo pia Mwenyezi Mungu alimtaka Mtume wake Muhammad SAW autake umma wake ulitekeleze. Ni matumaini yangu mtakuwa nami hadi mwisho wa dakika hizi za makala hii ya Amali Zilizo Bora.
*******
Katika kitabu cha al Mahasin imepokewa hadithi kutoka kwa Imam Ridha AS akisema: Mtu ambaye anapenda amwangalie Mwenyezi Mungu bila ya kizuizi na yeye aangaliwe na Mwenyezi Mungu bila ya kizuizi, basi awafanye Aali Muhammad SAW kuwa mawalii wake, na ajiweke mbali na maadui wao, na amtii Imam wa zama zake kutoka kwa Ahlul Bayt wa Mtume SAW.
Maana ya kumwangalia Mwenyezi Mungu hapa ni kuwa karibu mno na Allah na rehema Zake kama zinavyoashiria wazi wazi aya za Qur'ani Tukufu.
Na imepokewa hadithi kutoka katika kitabu hicho hicho cha al Mahasin kutoka kwa al Fadhil ambaye anasema: Nilimuuliza Abul Hasan ar Ridha AS: Kitu gani ambacho kinamkurubisha mno mja kwa Mwenyezi Mungu katika mambo ya faradhi? Akasema: Amali bora kabisa inayomkurubisha mja kwa Mola wake ni kumtii Allah na kumtii Mtume na kumpenda Allah na kumpenda Mtume SAW na wasimamizi wa haki wa mambo yenu.
Naye Imam Baqir AS alikuwa anasema: Kutupenda sisi Ahlul Bayt ni imani na kutuchukia ni kufru.
Aidha imepokewa hadithi katika kitabu hicho kutoka kwa Amiru Muuminin Ali bin Abi Talib AS kwamba alimwambia Abi Abdillahi al Judali kuwa: Je nikueleze jambo jema ambalo mtu akilitenda atasalimika na fadhaa ya Siku ya Kiyama na ovu ambalo akilitenda mja Mwenyezi Mungu atamvurumisha motoni? Nikasema: Naam. Akasema: Jema ni kutupenda sisi Ahlul Bayt na ovu ni kutuchukia sisi.
*******
Wapenzi wasikilizaji, aidha tunasoma katika kitabu cha Fiqhur Ridha kutoka kwa Imam huyo mtukufu akisema: Zidisheni kumsalia Mtume na Aali zake AS, na kuwaombea dua waumini wanaume na waumini wanawake nyakati za mchana na usiku. Kwani kumsalia Mtume na Aali zake ni bora ya amali njema. Jitoleeni haraka kuwakidhia waumini haja zao na kuingiza furaha nyoyoni mwao na kuwaondolea matatizo yao kwani hakuna jambo bora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu baada ya faradhi kuliko kuingiza furaha katika nyoyo za waumini. Msiache amali njema na jihadi katika ibada na kutawakali kupitia kuwapenda Aali Muhammad AS na msiache kuwapenda Aali Muhammad AS na kutii amri zao kupitia kutawakali kwa ibada, kwani halikubaliwi moja ya mawili hayo bila ya la pili lake.
Wassalaamu Alaykum Warahmatullahi Wabarakaatuh.


0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com