Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Russia: Iran ijumuishwe katika vita dhidi ya ugaidi

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Russia: Iran ijumuishwe katika vita dhidi ya ugaidiSergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa, nchi zote za Mashariki ya Kati ikiwemo Iran zinapasa kushirikishwa katika mapambano ya pamoja dhidi ya ugaidi. Lavrov ameongeza kuwa, ni muhimu kukabiliana na ugaidi na kwamba serikali za kieneo zinapaswa kushirikishwa kwenye vita hivyo ikiwemo serikali ya Iran na Syria.
Akiashiria hatua za Marekani za kupambana na ugaidi Mashariki ya Kati, Lavrov ameongeza kuwa, nchi zinazochukua hatua za upande mmoja kupambana na ugaidi kwenye eneo kiuhakika zinasababisha vitisho zaidi. Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia pia amesema kushindwa Washington kutathmini siasa zake katika muongo uliopita kumesababisha mgogoro unaoendelea sasa Mashariki ya Kati.
       

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com