Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Mwanaharakati wa haki za binadamu akamatwa Bahrain

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Mwanaharakati wa haki za binadamu akamatwa BahrainPolisi ya Bahrain imemtia mbaroni mwanaharakati maarufu wa haki za binadamu Nabeel Rajab kutokana na kuandika katika mtandao wa Twitter matamshi ya kupinga serikali, huku utawala wa Manama ukiendelea kuwakandamiza waandamanaji. Taarifa iliyotolewa na serikali imeeleza kuwa, baada ya polisi kumhoji mwanaharakati huyo ambaye ni mkurugenzi wa Kituo cha Haki za Binadamu cha Bahrain (BCHR), hatua zimechukuliwa za kumfikisha mahakamani.
Katika moja ya matamshi yake kwenye mtandao wa Twittr Nabeel Rajab alisema kuwa, Wabahraini waliojiunga na kundi la Daesh nchini Syria na Iraq kiuhakika wanatoka katika taasisi za usalama za utawala wa kifalme wa Manama.
Makundi ya haki za binadamu yamelaani kukamatwa mwanaharakati huyo na kuutaka utawala wa kifalme wa al Khalifa uache kuwanyanyasa watetezi wa haki za binadamu.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com