Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Thursday, October 2

Michezo ya mataifa ya Asia: Timu ya Kabaddi ya Iran ya wanaume yatinga fainali

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Michezo ya mataifa ya Asia: Timu ya Kabaddi ya Iran ya wanaume yatinga fainaliTimu ya taifa ya Kabaddi ya Iran kwa upande wa wanaume imejikatia tiketi ya fainali ya mchezo huo katika mashindano ya mataifa ya Asia yanayoendelea katika mji wa Incheon nchini Korea Kusini. Iran ambayo imeonekana tishio katika mchezo huo, imetinga fainali kwa kishindo baada ya kuigaragaza Pakistan kwa pointi 25 kwa 14 Kabla ya mchezo huo India nayo ilikuwa imefanikiwa kukata tiketi ya kutumbukia fainali katika mchezo hyuo wa Kabaddi baada ya kuwabwaga wenyeji Korea Kusini katika mechi ya nusu fainali. Kwa msingi huo, wacheza Kabaddi wa Iran watagaragazana na India katika mechi ya fainali inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Fainali hiyo itakumbusha fainali ya mcxhezo huo katika mashindano yaliyopita ya Guangzhou ambapo Iran ilishindwa na India katika mchezo huo na kukosa medali ya dhahabu. Timu ya taifa ya Iran ya Kabaddi kwa upande wa akina dada nayo imetinga fainali ya mchezo huo baada ya kuwapeleka mchakamchaka akina dada wa Bangladesh katika mchezo wa nusu fainali. Kama ilivyo kwa wanawaume, akinana dada wa Iran pia wanachuana na wale wa India katika kuwania medali ya dhahabu

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com