Siku kama ya leo miaka 120 iliyopita yaani tarehe 15 Oktoba mwaka 1894, ilianza kesi ya Alfred Dreyfus mjini Paris, Ufaransa. Dreyfus alikuwa afisa wa jeshi la Ufaransa mwenye asili ya Kiyahudi ambaye kesi yake ni miongoni mwa matukio yaliyozusha makelele mengi katika karne ya 19 nchini humo. Afisa huyo wa jeshi alituhumiwa kuisaliti nchi yake na kutoa siri za jeshi la Ufaransa kwa Ujerumani. Alivuliwa cheo chake na akahukumiwa kifungo cha maisha jela. Baada ya kuhukumiwa kifungo hicho, ilithibitika kwamba Alfred Dreyfus hakuwa na hatia yoyote. Kwa utaratibu huo aliachiwa huru na kurejeshewa heshima na vyeo vyake. Hukumu ya kifungo cha maisha jela ya Dreyfus na kisha kutambuliwa kwake kuwa hakuwa na hatia, kadhia ambayo inatambuliwa kwa jina la Dreyfus Affair, ilitumiwa na Wazayuni katika propaganda za urongo kudai kwamba Wayahudi wamedhulumiwa barani Ulaya. Wazayuni walitumia vibaya kadhia hiyo kujiimarisha zaidi.
Tarehe 15 Oktoba miaka 170 iliyopita alizaliwa mwanafalsafa wa Kijerumani Friedrich Wilhelm Nietzsche. Baada ya kuhitimu masomo, Nietzsche alianza kufunza katika Chuo Kikuu cha Basel. Mwanafalsafa huyo alikuwa akipinga dini na misingi ya kimaadili na katika falsafa na mitazamo yake alikuwa akiamini nadharia ya "Superman", kwa maana ya mtu mwenye uwezo kupita kiasi. Nietzsche alikuwa akiamini kwamba, mtu mwenye uwezo kupita kiasi au Superman ni matokeo ya irada na matashi ya mwanadamu na huwa juu ya mema na mabaya yote. Mwanafalsafa huyo ameandika vitabu kadhaa ikiwa ni pamoja na Beyond Good and Evil, The Birth of Tragedy na Thus Spoke Zarathustra. Katika kipindi cha mwishoni mwa uhai wake Friedrich Wilhelm Nietzsche alipoteza mlingano wa kifikra na alifariki dunia mwaka 1900.
Na siku kama ya leo miaka 32 iliyopita, mwakilishi wa Imam Khomeini M.A na Imam wa Sala ya Ijumaa ya mji wa Kermanshah huko magharibi mwa Iran Ayatullah Ashrafi Isfahani, aliuawa shahidi na vibaraka wa kundi la MKO akiwa katika mihrabu ya ibada. Ayatullah Ashrafi Isfahani aliongoza wananchi wa Kermanshah katika harakati na mapambano ya Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya utawala wa Shah. Aliteuliwa na Imam Khomeini kuwa Imam wa Sala ya Ijumaa ya Kermanshah baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini na aliuawa shahidi katika mihrabu akisalisha Sala ya Ijumaa
0 toamaon yako: