Leo ni Jumanne tarehe 19 Dhilhaji 1435 Hijria sawa na 14 Oktoba 2014.

Siku kama ya leo miaka 61 iliyopita Wazayuni wa Israel walivamia kijiji cha Qibya kilichoko katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan huko Palestina na kufanya jinai kubwa za kutisha. Katika mashambulizi na uvamizi ulioendelea katika kijiji hicho kwa muda wa siku mbili, Wazayuni walifanya mauaji na ukatili mkubwa dhidi ya raia wa Kipalestina wasio na hatia. Mbali na Wazayuni hao kuwaua na kuwajeruhi kwa umati raia zaidi ya 42 wa Kipalestina, askari wa Israel waliokuwa wakiongozwa na waziri mkuu wa zamani wa utawala huo wa kigaidi Ariel Sharon walibomoa makumi ya nyumba na shule za kijiji hicho. Mauaji hayo ya halaiki ni miongoni mwa mifano ya ugaidi wa utawala ghasibu wa Israel hususan waziri mkuu wa zamani wa utawala huo Ariel Sharon.
Na tarehe 19 Dhulhija mwaka 1257 Hijria alizaliwa Ayatullah Sayyid Muhammad Tabatabai, mmoja wa wasomi wakubwa wa Kiislamu na wapigania uhuru wa Iran. Wakati wa mapinduzi ya kikatiba nchini Iran, Sayyid Muhammad Tabatabai alikuwa akihesabika kuwa miongoni mwa viongozi wakubwa wa mapinduzi hayo. Tabatabai alishirikiana na Sayyid Abdullah Behbahani ambaye naye alikuwa mmoja wa viongozi wa harakati ya kikatiba dhidi ya utawala wa Qajari nchini Iran.
Mbali na kupigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, Sayyid Tabatabai alikuwa mwanazuoni hodari na alifanya bidii kubwa kueneza mafundisho ya Kiislamu
0 toamaon yako: