Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Monday, October 20

Alkhamisi, 16 Oktoba, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Leo ni Alkhamisi tarehe 21 Dhulhaji 1435 Hijria sawa na tarehe 16 Oktoba 2014.
Alkhamisi, 16 Oktoba, 2014Siku kama ya leo tarehe 24 Mehr miaka 36 iliyopita, kulitokea maafa makubwa kwenye Msikiti Mkuu wa Kerman, huko amagharibi mwa Iran baada ya vikosi vya polisi na usalama vya utawala wa mfalme Muhammad Reza Pahlavi kuwashambulia kwa risasi wananchi waliokusanyika kwenye eneo hilo la msikitini kwa shabaha ya kuadhimisha 40 ya mashahidi waliouawa tarehe 17 Shahrivar mjini Tehran. Shambulio hilo la vikosi vya usalama vya Shah liliamsha hasira na wimbi jipya la harakati za wananchi za kupinga utawala kibaraka wa Mfalme Muhammad Reza Pahlavi.
Miaka 68 iliyopita katika siku kama ya leo, mwafaka na tarehe 16 Oktoba 1946, kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa na Mahakama ya Nuremberg walinyongwa viongozi 9 wa Ujerumani ya Wanazi baada ya kupatikana na hatia za kutenda jinai za kivita. Herman Goering aliyekuwa Kamanda Mkuu wa kikosi cha jeshi la anga la Ujerumani na msaidizi wa dikteta Adolphe Hitler ambaye alikuwa amehukumiwa adhabu ya kifo, pia aliamua kujinyonga yakiwa yamebakia masaa machache kabla ya kutekelezwa hukumu hiyo ya kifo. Hali kadhalika mahakama hiyo iliwahukumu adhabu ya kifungo cha muda mrefu viongozi wengine 9 wa Ujerumani ya Wanazi na wengine watatu hawakupatikana na hatia. Mahakama ya Nuremberg iliyoundwa na wawakilishi wa Marekani, Urusi ya zamani, Uingereza na Ufaransa kwa shabaha ya kuwahukumu maafisa 22 wa Manazi wa Ujerumani kwa tuhuma za kufanya jinai za kivita ilikamilisha shughuli zake tarehe 30 Septemba mwaka 1946.
Na miaka 867 iliyopita sawa na tarehe 21 Dhulhija mwaka 568 Hijria, alizaliwa Abulhassan Ali Bin Yusuph Sheibani maarufu kwa jina la 'Ibn Qefti, ambaye alikuwa mwandishi hodari wa Kiislamu katika mji mdogo wa Qeft nchini Misri. Baada ya kumaliza masomo alijishughulisha na kazi ya uhakimu. Ibn Qefti ameandika vitabu 26 vya kihistoria na kisayansi na mashuhuri zaidi ni kile alichokipa jina la Tarikhul Hukamaa. Mwandishi huyo wa Kiislamu alifariki dunia mwaka 649 Hijria.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com