Abdul Malik al Houthi kiongozi wa harakati ya Ansarullah, amesema katika ujumbe wake kwa taifa la Yemen kuwa, wananchi ndio washindi wa mapinduzi ya nchi hiyo. Amesema, makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali na wapinzani wa Yemen, hayajafanya upande wowote ushinde au ushindwe bali wananchi ndio washindi, kwa kuwa walifanya harakati ili kufikia matakwa yao halali na ya kisheria. Hapana shaka kuwa, hali iliyojitokeza katika kipindi cha wiki 3 zilizopita nchini Yemen ilikuwa ni ya kimapinduzi. Baadhi ya duru za kisiasa pia zimesema kuwa, maandamano ya hivi karibuni ni muendelezo wa harakati za kimapinduzi zilizoanzishwa na wananchi wa Yemen mwaka 2011. Kwa vyovyote vile, ni wazi kuwa, mara hii pia Wayemen bila kubeba silaha wamefanikiwa kufikia matakwa yao na kuilazimisha serikali ya Abd Rabbuh Mansur Hadi kusalimu amri. Muhammad Basindawa, Waziri Mkuu wa Yemen siku kadhaa zilizopita alijiuzulu na kikosi cha kwanza ya jeshi la Yemen kinaendelea kukabidhi silaha zake kwa wanaharakati wa kundi la Houthi huku vikosi vilivyoundwa na wananchi vikichukua jukumu la kuimarisha nidhamu na usalama nchini humo. Kwa hivi sasa jambo linaloshuhudiwa wazi ni kuwa, wapinzani na hasa kundi la Ansarullah na harakati ya Houthi wamefanikiwa kudhibiti hali ya mambo kiasi kwamba na Rais Abd Rabbuh Mansur Hadi hivi sasa hana njia nyingine isipokuwa kuheshimu makubaliano ya usitishaji mapigano. Imekubaliwa kuwa katika kipindi cha wiki moja au mbili zijazo serikali mpya ya Yemen iundwe, itakayokuwa nembo ya umoja wa kitaifa na kushirikisha makundi yote ya kisiasa. Wapinzani wa Yemen kwa sasa sambamba na kusimamia mageuzi yote wanafuatilia kwa karibu harakati za viongozi wa nchi hiyo. Miongoni mwa matakwa ya wananchi ni kukomeshwa ulaji rushwa na kukabiliana na ufisadi na ubadhirifu nchini Yemen, na wanamtaka Abd Rabbuh Mansur Hadi ayatimize. Katika siku zilizopita baadhi ya viongozi mafisadi wa Yemen walikimbia nchi kutokana na hofu ya hasira za wananchi huku habari zikieleza kwamba, wanapinduzi walivamia nyumba za maafisa wenye mfungamano na Ali Abdallah Swaleh dikteta wa zamani wa Yemen. Hali ilivyo hivi sasa kamwe si kwa maslahi ya viongozi wa serikali wa Sana'a, na ndio maana viongozi wa nchi hiyo wanajizuia kufanya jambo lolote litakaloamsha tena hasira za wananchi. Hasa kwa kuzingatia kuwa mji mkuu wa Yemen unadhibitiwa na wanamgambo wa Houthi. Katika miaka ya hivi karibuni kundi la Houthi lilikuwa limetengwa kisiasa, na sio tu halikuwa na nafasi katika muundo wa serikali ya Yemen bali serikali ya Sana'a kila mara ilianzisha vita dhidi ya kundi hilo kwa visingizo tofauti. Hata hivyo inaonekana kuwa, kundi la Houthi lina uungaji mkono mkubwa wa wananchi wa Yemen na limefanikiwa kuanzisha mwamko, ambao pengine hata Abd Rabbuh Mansur Hadi hakudhani ungefanikiwa. Kwa msingi huo, fursa muwafaka imepatikana kwa manufaa ya Wahouthi na harakati ya Answarullah ya Yemen. Fursa ambayo Wahouthi na wapinzani kamwe hawataki kuipoteza. Kiongozi wa harakati ya Answarullah Abdul Malik Houthi kwa sasa anataka matatizo yote yaliyoko nchini humo yatafutiwe ufumbuzi. Ameiambia serikali ya Sana'a kuwa, mapambano bado yanaendelea. Suala hilo linamaanisha kuwa, kusainiwa tu makubaliano ya usitishaji mapigano hakuna maana ya kufikia tamati mapinduzi ya wananchi nchini Yemen.Abdul Malik al Houthi kiongozi wa harakati ya Ansarullah, amesema katika ujumbe wake kwa taifa la Yemen kuwa, wananchi ndio washindi wa mapinduzi ya nchi hiyo. Amesema, makubaliano yaliyofikiwa kati ya serikali na wapinzani wa Yemen, hayajafanya upande wowote ushinde au ushindwe bali wananchi ndio washindi, kwa kuwa walifanya harakati ili kufikia matakwa yao halali na ya kisheria. Hapana shaka kuwa, hali iliyojitokeza katika kipindi cha wiki 3 zilizopita nchini Yemen ilikuwa ni ya kimapinduzi. Baadhi ya duru za kisiasa pia zimesema kuwa, maandamano ya hivi karibuni ni muendelezo wa harakati za kimapinduzi zilizoanzishwa na wananchi wa Yemen mwaka 2011. Kwa vyovyote vile, ni wazi kuwa, mara hii pia Wayemen bila kubeba silaha wamefanikiwa kufikia matakwa yao na kuilazimisha serikali ya Abd Rabbuh Mansur Hadi kusalimu amri. Muhammad Basindawa, Waziri Mkuu wa Yemen siku kadhaa zilizopita alijiuzulu na kikosi cha kwanza ya jeshi la Yemen kinaendelea kukabidhi silaha zake kwa wanaharakati wa kundi la Houthi huku vikosi vilivyoundwa na wananchi vikichukua jukumu la kuimarisha nidhamu na usalama nchini humo. Kwa hivi sasa jambo linaloshuhudiwa wazi ni kuwa, wapinzani na hasa kundi la Ansarullah na harakati ya Houthi wamefanikiwa kudhibiti hali ya mambo kiasi kwamba na Rais Abd Rabbuh Mansur Hadi hivi sasa hana njia nyingine isipokuwa kuheshimu makubaliano ya usitishaji mapigano. Imekubaliwa kuwa katika kipindi cha wiki moja au mbili zijazo serikali mpya ya Yemen iundwe, itakayokuwa nembo ya umoja wa kitaifa na kushirikisha makundi yote ya kisiasa. Wapinzani wa Yemen kwa sasa sambamba na kusimamia mageuzi yote wanafuatilia kwa karibu harakati za viongozi wa nchi hiyo. Miongoni mwa matakwa ya wananchi ni kukomeshwa ulaji rushwa na kukabiliana na ufisadi na ubadhirifu nchini Yemen, na wanamtaka Abd Rabbuh Mansur Hadi ayatimize. Katika siku zilizopita baadhi ya viongozi mafisadi wa Yemen walikimbia nchi kutokana na hofu ya hasira za wananchi huku habari zikieleza kwamba, wanapinduzi walivamia nyumba za maafisa wenye mfungamano na Ali Abdallah Swaleh dikteta wa zamani wa Yemen. Hali ilivyo hivi sasa kamwe si kwa maslahi ya viongozi wa serikali wa Sana'a, na ndio maana viongozi wa nchi hiyo wanajizuia kufanya jambo lolote litakaloamsha tena hasira za wananchi. Hasa kwa kuzingatia kuwa mji mkuu wa Yemen unadhibitiwa na wanamgambo wa Houthi. Katika miaka ya hivi karibuni kundi la Houthi lilikuwa limetengwa kisiasa, na sio tu halikuwa na nafasi katika muundo wa serikali ya Yemen bali serikali ya Sana'a kila mara ilianzisha vita dhidi ya kundi hilo kwa visingizo tofauti. Hata hivyo inaonekana kuwa, kundi la Houthi lina uungaji mkono mkubwa wa wananchi wa Yemen na limefanikiwa kuanzisha mwamko, ambao pengine hata Abd Rabbuh Mansur Hadi hakudhani ungefanikiwa. Kwa msingi huo, fursa muwafaka imepatikana kwa manufaa ya Wahouthi na harakati ya Answarullah ya Yemen. Fursa ambayo Wahouthi na wapinzani kamwe hawataki kuipoteza. Kiongozi wa harakati ya Answarullah Abdul Malik Houthi kwa sasa anataka matatizo yote yaliyoko nchini humo yatafutiwe ufumbuzi. Ameiambia serikali ya Sana'a kuwa, mapambano bado yanaendelea. Suala hilo linamaanisha kuwa, kusainiwa tu makubaliano ya usitishaji mapigano hakuna maana ya kufikia tamati mapinduzi ya wananchi nchini Yemen.
IQRA FM RADIO
Wednesday, September 24
Browse: Home
» Habari za kitaifa na kimataifa
» Wananchi wa Yemen ndio washindi wa mapinduzi ya nchi yao
Wananchi wa Yemen ndio washindi wa mapinduzi ya nchi yao
Posted by mkachu |  Tagged as: Habari za kitaifa na kimataifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Andika Maoni
add
LEO KATIKA HISTORIA
TANGAZANASI
kwama Matangazo wasiliana nasi kupitia anuani zifuataz
Email:
iqrafmradio@gmail.cm
contact us:
0752925259
0762118805
infohttp:iqrafmradio.blogspot.com
uimara wa redio iqra upo mikononi mwako
>>Wote mnakalibishwa.....................................
Email:
iqrafmradio@gmail.cm
contact us:
0752925259
0762118805
infohttp:iqrafmradio.blogspot.com
uimara wa redio iqra upo mikononi mwako
>>Wote mnakalibishwa.....................................
ZILIZO SOMWA ZAIDI
-
Mwenyezi Mungu anasema: Niombeni nitakupeni. Zifuatazo hapa ni dua za baada ya nyakati mbalimbali za sala. Tunamuomba Mwenyezi Mung...
-
Mwenyezi Mungu anasema: Niombeni nitakupeni. Zifuatazo hapa chini ni dua 25 za Qur'ani Tukufu tulizozinukuu kutoka katika...
-
RATIBA YA VIPINDI KWA JUMA ZIMA RATIBA - JUMATATU MUDA KIPINDI MUHUSIKA 06:30-07:00 M...
-
Rais Bashar al-Assad wa Syria amesema kuwa, kuna udharura wa kuweko vita vya kimataifa dhidi ya magaidi. Rais Assad amesisitiza kwamba, kwa...
MITANDAO YA KIJAMII
TAFUTA HABARI ZILIZO SOMWA NYUMA
Powered by Blogger.
Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...
0 toamaon yako: