
Askofu Josef Wesolowski askofu mkuu wa zamani na balozi wa zamani wa Vatican katika Jamhuri ya Dominican
skofu Mkuu wa zamani wa Kanisa Katoliki amepewa adhabu ya kifungo cha nyumbani, baada ya kukabiliwa na tuhuma za kuwadhalilisha na kuwanyanyasa watoto kijinsia.
Federico Lombard Msemaji wa Vatican amesema kuwa Josef Wesolowski askofu mkuu wa zamani na balozi wa zamani wa Vatican katika Jamhuri ya Dominican, amepewa adhabu hiyo kutokana na amri iliyotolewa na Papa Francis Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani.
Askofu Mkuu Wesolowski amekumbwa na kashfa ya kuwanyanyasa kijinsia watoto kwa kuwarubuni kwa pesa, wakati alipokuwa balozi wa Vatican katika Jamhuri ya Dominican.
Hivi karibuni, Vatican ilitoa takwimu zinazoonyesha kwamba katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, maaskofu 848 walijihusisha na vitendo vya ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto wasiopungua 2,572 duniani kote.
Wakati huohuo, Baraza la Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imezikosoa vikali sera za Vatican za kuwahamisha maaskofu na makasisi waliotenda jinai kutoka kituo kimoja hadi kingine kwa lengo la kuficha jinai na ufuska wao.
0 toamaon yako: