Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Wednesday, September 24

Obama aomba ushirikiano dhidi ya IS

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Rais Obama anataka mataifa ya magharibi kushirikiana katika vita dhidi ya Islamic State
Rais wa Marekani Barack Obama ametumia hotuba yake katika kikao cha baraza la Umoja wa Mataifa kuomba ushirikiano wa mataifa mengine katika vita dhidi ya kile alichokitaja kama mtandao wa chuki, mauaji na uhasama.
Matamshi ya Obama yalilenga kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Islamic State nchini Syria.
Rais Obama, amesema kuwa Marekani itatumia nguvu kwa ushirikiano na washirika wake na kuwafunza pamoja na kuwapa silaha wanajeshi wanaopambana na I-S , wakati ufadhili wa kundi hilo ukiangamizwa.
Rais Obama atakuwa mwenyekiti wa mkutano wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa utakaofanyika baadaye mwaka 2000.
Alisema kuwa watafikia azimio ambalo litaeleza jukulu la kila nchi katika kupambana na uenezwaji wa itikadi kali ambao unaambatana na ghasia.
Awali, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon, alizungumzia unyama unaotendwa na kundi la Islamic State na alichokiita mauaji yanayoendelezwa na wapiganaji wa Boko Haram.
Wapiganaji wa Islamic State
Wakati huohuo, ndege za kivita za Marekani zimefanya mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa Islamic State nchini Iraq na Syria, na kuharibu magari na maeneo yenye silaha.
Taarifa hii ni kwa mujibu wa jeshi la Marekani.
Magari manane ya IS yaliharibiwa karibu na eneo la Abu Kamal upande wa mpaka wa Syria na Iraq pamoja na maeneo mengine mawili ya Deir al-Zour Mashariki mwa Syria.
Nchini Iraq, mashambulizi yalifanywa dhidi ya IS Magharibi mwa Baghadad na Kusini Mashariki mwa Irbil karibu na eneo la Kikurdi.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com