
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imeeleza wasiwasi wake kuhusiana na tatizo la chakula linalowakabili malefu ya wakimbizi wa Somalia. Kristy Manners afiwa wa shirika hilo nchini Somalia amesema kuwa, mazao machache, ukame na pia migogoro ya ndani imewalazimisha wakazi wengi wa eneo la Hiiran kuyakimbia makaazi yao na kuwa wakimbizi kwenye eneo la Beletweyne. Jana shirika hilo la misaada liligawa chakula kwa karibu wakimbizi 36,000 katika eneo la Beletweyne nchini Somalia.
Afisa huyo wa Red Cross amesisitiza kuwa, ingawa hatua ya pili ya kugawa chakula kwa wakimbizi 36 elfu katika mwaka huu wa 2014 imemalizika, lakini wakimbizi wa Somalia bado wanahitajia misaada ya chakula.
Takwimu mpya za Umoja wa Mataifa katika miezi 8 ya mwaka huu zinaonesha kuwa, Wasomali 107, 000 wanaishi kama wakimbizi ndani ya nchi yao, huku wengine karibu 23 elfu wakipata hifadhi katika nchi za Yemen, Kenya na Ethiopia
0 toamaon yako: