Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 21

Waliotaka kujitawala Scotland washindwa

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa Wascoti waliokuwa wakipinga uhuru na kujitawala kwa eneo hilo kutoka Muungano wa Ufalme wa Uingereza wameshinda kwa asilimia 55.42 ya kura katika kura ya maoni iliyopigwa siku ya Alkhamisi. Watu karibu milioni 4.29 ambao ni asilimia 97 ya jamii ya watu wa Scotland walikuwa wamejiandikisha kushiriki katika kura hiyo ya maoni iliyolenga kuainisha mustakbali wa Muungano Waliotaka kujitawala Scotland washindwawa Ufalme wa Uingereza uliodumu kwa miaka 307. Mara tu baada ya kutangazwa matokeo ya awali, Alex Salmond, Waziri wa Kwanza wa Scotland na ambaye pia ni kiongozi wa mrengo wa wanaopigania uhuru wa eneo hilo kutoka muungano wa Uingereza alikubali kushindwa katika kura hiyo ya maoni na wakati huohuo kuitaka serikali ya London itekeleze haraka ahadi ilizotoa kwa eneo hilo kwa kulipatia mamlaka zaidi ya kujitawala. Salmond Amesema kwa sasa wananchi waliowengi wa Scotland wameamua eneo hilo lisijitenge na Uingereza na kuwa nchi huru. Scotland ambayo ina akiba kubwa ya mafuta katika maji yake ya Bahari ya Kaskazini inaunda Muungano wa Ufalme Uingereza pamoja na maeneo mengine ya England, Wales na Ireland Kaskazini. Baada ya kutangazwa matokeo ya kura ya maoni kwa hivi sasa inaonekana kuwa mvutano uliokuwepo kati ya waungaji mkono na wapinzani wa kujitenga Scotland na muungano wa Uingereza umekwisha. Kwa kuzingatia kuwa idadi ya waungaji mkono wa kujitawala Scotland imeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni, jambo hilo limewatia wasiwasi mkubwa watawala wa Uingereza na hasa Waziri Mkuu David Cameron ambaye hivi karibuni alitoa ahadi chungu nzima za kuwapa mamlaka zaidi Wascoti ili kuwashawishi wasijitenge na kujitawala wenyewe. Wakati huohuo alizungumza kwa maneno makali na kuwaonya waungaji mkono wa kujitenga eneo hilo waache kufuatilia suala hilo la sivyo wakabiliwe na matokeo mabaya.
Licha ya matokeo hayo kuwa kwa maslahi ya wapinzani wa kujitenga Scotland, lakini ni wazi kuwa yamewagawa watu wa eneo hilo katika makundi mawili tofauti yanayokaribiana kiidadi. Kundi la kwanza linaona kuwa linataka kuwa na maisha bora kwa kuendelea kubakia katika muungano wa Uingereza na la pili linataka kufikia ndoto yake ya muda mrefu ya kujitawala na hivyo kuacha mashindano ya muda mrefu ya kihistoria, kijografia, kiutamaduni, kimadhehebu na kisiasa na England. Mashindano hayo yalipata kasi na nguvu zaidi tokea miaka 50 iliyopita. Takriban nusu ya Wascoti hujitambulisha kuwa wao ni Wascoti kwanza kabla ya kufikiria kujitambulisha kuwa ni Waingereza. Kwa kuzingatia kuwa waliotaka uhuru wa Scotland wameshindwa kwa kura chache tu, ni wazi kuwa wanawachukulia wapinzani wao kuwa ndio waliowakosesha fursa ya kihistoria ya kujitawala na kwa hivyo hawataacha kupigania kuthibiti kwa ndoto yao ya kujitawala kwa eneo hilo. Ni wazi kuwa wanaotaka uhuru wa Scotland wanaona kuwa wameshindwa katika kura hii ya maoni kutokana na zaidi ya nusu ya watu wa eneo hilo kuamini ahadi zilizotolewa na serikali ya London.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com