Mwakilishi maalumu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu nchini Sudan
amesema kuwa, taasisi hiyo inaunga mkono mazungumzo ya kitaifa nchini
humo. Swalah Halima pia ameyataka makundi yenye kubeba silaha na vyama
vya upinzani kujiunga na mazungumzo hayo na serikali, ili kutatua
matataizo ya kisiasa ya nchi hiyo. Aidha amesifu mpango huo wa mazungumo
ya kitaifa uliobuniwa na Rais Omar al Bashir na kusema kwamba, maafisa
wa Khartoum wamepiga hatua chanya kwa ajili ya kuandaa mazingira ya
mazungumzo.Hayo yanajiri huku ikiripotiwa kuwa idadi kubwa ya waasi wa magharibi mwa Sudan wanatarajiwa kutia saini makubaliano ya amani na serikali. Jaafar Abdulhakim kamanda wa jimbo la Darfur amesema kuwa, idadi kubwa ya wanamgambo wa kundi la waasi wa Harakati ya Ukombozi wa Sudan wamejitenga na kundi hilo na kwamba hivi karibuni watatia saini makubaliano ya amani na serikali ya Khartoum.

Facebook
Twitter
RSS
0 toamaon yako: