
Shirika la Kilimo na Chakula Duniani FAO limetangaza kuwa, zaidi
ya watu milioni 800 wanakabiliwa na balaa la njaa duniani. Taarifa
iliyotolewa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa inaeleza kuwa, katika
kila watu tisa mmoja wao anakabiliwa na balaa la njaa duniani. Shirika
la FAO limeeleza kuwa, idadi ya watu waliokumbwa na balaa la njaa katika
kipindi cha miaka 10 iliyopita ilipungua kwa karibu watu milioni 100
ikilinganishwa na mwaka 1990 ambapo ilikuwa karibu watu milioni 200.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, nchi nyingi za Kiafrika na hasa zilizoko
katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara barani humo, zinakabiliwa na
balaa hilo. Imeelezwa kuwa, watu milioni 214 wanakabiliwa na balaa la
njaa barani Afrika. Shirika la Kilimo na Chakula Duniani limeeleza kuwa,
nchini Somalia pekee, zaidi ya watu milioni moja wanakabiliwa na balaa
la njaa.
0 toamaon yako: