Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesema kuwa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu vimeongezeka sana nchini humo.
Ripoti iliyotolewa na ofisi hiyo imesema kuwa jumla ya kesi 257 za ukandamizaji wa haki za binadamu ziliripotiwa Congo DR mwezi Agosti mwaka huu pekee. Ripoti hiyo imesema wahanga wa vitendo hivyo wameongezeka kutoka 405 na kufikia 638 ndani ya mwezi huo wa Agosti. Ofisi hiyo ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imesisitiza kuwa, kiwango cha ukiukwaji wa haki za binadamu ndani ya mwezi huu wa Septemba kimeongezeka kwa asilimia 58 ukilinganisha na mwezi uliopita. Mikoa ya Kasaï-Oriental, Kivu Kaskazini na Kusini ndiko kunakotajwa kukithiri sana vitendo hivyo. Ofisi hiyo imewataja maafisa wa serikali ya Kinshasa kuwa wanahusika na kesi hizo kwa asilimia 57, huku makundi ya wanamgambo wakihusishwa kwa asilimia 43.
0 toamaon yako: