Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, njama za vikwazo dhidi ya Iran zimefeli vibaya na hakuna uwezekano wa hali kurejea kama ilivyokuwa mwaka mmoja uliopita. Rais Rouhani ameyasema hayo wakati alipokutana na Wairan waishio nchini Marekani ambapo sanjari na kuashiria makubaliano kati ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kundi la 5+1 kuhusu ratiba ya hatua za pamoja huko Geneva, Uswis amesema: “Ni suala la kufurahisha kwamba, mtazamo wa ulimwengu wa leo juu ya serikali na mfumo wa Iran umebadilika.” Akifafanua mafanikio na maendeleo ya serikali ya awamu ya 11 katika nyuga mbalimbali, amesema kuwa, mafanikio muhimu ya serikali ni kurejesha usalama na uthabiti wa uchumi nchini Iran, jambo ambalo linatoa mustakbali mwema na rkuwavutia wawekezaji.
Rais Hassan Rouhani yuko nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki katika kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo pia amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa nchi mbalimbali.
0 toamaon yako: