Wizara ya Waqfu ya Syria imeitaja hatua ya Saudi Arabia ya kuwazuia raia wa Syria kushiriki katika ibada ya Hija kuwa inabainisha uadui wa wazi wa Riyadh kwa taifa hilo. Wizara hiyo imelaani hatua hiyo ya utawala wa Saudia ikisema kuwa haikubalika na inaonesha ushirikiano wa wazi kati ya Riyadh na madola ya Kimagharibi hasa Marekani dhidi ya Syria. Wizara ya Waqfu ya Syria imesisitiza kuwa, marufuku hiyo ya kidhalimu haina mfano katika kipindi chote cha historia ya umma wa Kiarabu na Kiislamu.
Ni vyema kuashiria hapa kwamba, hii ni mara ya tatu mtawalia ambapo utawala wa kifalme wa Saudi Arabia unawazuia raia wa Syria kushiriki katika ibada ya hija, tangu kulipoibuka machafuko katika nchi Syria.


Facebook
Twitter
RSS
0 toamaon yako: