Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Friday, September 26

Rais H. Mohamud: Jamii ya kimataifa iisaidie Somalia

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Rais H. Mohamud: Jamii ya kimataifa iisaidie SomaliaRais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia ameitaka jamii ya kimataifa kuizingatia kimisaada nchi yake kutokana na hali mbaya inayolikabili taifa hilo. Rais Mohamud ameyasema hayo katika hotuba aliyoitoa mbele ya kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, na kuongeza kuwa, hali ya kibinaadamu nchini mwake ni mbaya sana. Alisema kuwa ili kukabiliana na hali hiyo serikali ya Mogadishu inahitajia msaada wa kifedha wa takriban dola nusu bilioni. Alisema kuwa, watu milioni tatu na laki mbili wanahitajia msaada wa haraka nchini Somalia huku karibu watu milioni moja wengine wakikabiliwa na mgogoro wa chakula. Rais wa Somalia ameongeza kuwa, hadi sasa nchi yake bado imepokea nusu pekee ya misaada ya kimataifa iliyoahidiwa. Aidha amesisitizia umuhimu wa maendeleo ya kuimarisha usalama nchini humo na kusema kuwa, hii leo Somalia si nchi inayoweza kushindwa tena na ash-Shabab. Itakumbukwa kuwa, mwaka 2011 Somalia ilikumbwa na baa la njaa lililosababishwa na ukame, na kupelekea idadi kubwa ya watu kupoteza maisha.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com