Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Friday, September 26

Jumamosi, Septemba 27, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as: ,


Leo ni Jumamosi tarehe Pili Mfunguo tatu Dhil-Hijja 1435 Hijria sawa na tarehe 27 Septemba 2014 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 33 iliyopita wapiganaji shujaa wa Iran walifanikiwa kuvunja mzingiro wa mji wa Abadan katika operesheni ya haraka na iliyokuwa imeratibiwa vyema dhidi ya ngome za jeshi la Saddam Hussein. Operesheni hiyo ilitekelezwa na wapiganaji wa Iran kufuatia agizo la kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Imam Khomeini Mwenyezi Mungu amrehemu. Mji wa Abadan ulikuwa umezingirwa na wanajeshi wa Iraq kwa karibu mwaka mmoja tangu kuanza vita vya kulazimishwa vya utawala wa dikteta Saddam dhidi ya Iran. ***
Katika siku kama ya leo miaka 65 iliyopita, mji wenye jamii kubwa ya watu wa Beijing ulichaguliwa rasmi kuwa mji mkuu wa Uchina. Mji wa kihistoria wa Beijing unapatikana mashariki kwa nchi hiyo na unahesabiwa kuwa moja ya vituo vikubwa vya kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni vya China. Beijing ulichaguliwa kuwa mji mkuu wa China baada ya Mao Tse-tung kuchukua madaraka ya nchi na kiongozi wa wakati huo wa China Chiang Kai-shek akakimbilia Taiwan. ***
Miaka 73 iliyopita katika siku kama ya leo, jeshi la Ujerumani ya Kinazi lilipata ushindi mkubwa wakati lilipokuwa likisonga mbele kuelekea huko Urusi ya zamani katika vita vilivyokuwa vimeanza mwezi Juni mwaka 1941. Wanajeshi wa Urusi ya zamani walikabiliwa na mashambulizi ya pande zote ya vikosi vya Ujerumani wakati wakiwa wamechoka na kuishiwa zana za kivita. Mapigano kati ya pande mbili hizo yalipelekea kutekwa nyara wanajeshi wa Urusi ya zamani zaidi ya laki sita na kuharibiwa karibu vifaru 1200 na mizinga 5400 ya nchi hiyo. ***
Na miaka 18 iliyopita katika siku kama ya leo, kundi la Taliban lilivamia na kutwaa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul. Kundi hilo liliasisiwa mwaka 1994 na likateka hatua kwa hatua maeneo ya kusini na magharibi mwa Afghanistan kwa himaya ya Marekani, misaada ya kisiasa na kijeshi ya Pakistan pamoja na misaada ya kifedha ya Saudi Arabia. Jeshi la serikali ya Afghanistan lililokuwa likiongozwa na Ahmad Shah Mas'ud liliondoka mjini Kabul siku moja kabla ya Taliban kuuteka mji huo. Baada ya kuingia Kabul, kundi la Taliban lilianza kutekeleza sheria kali na zinazoshabihiana na zile za karne za kati dhidi ya wananchi.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com