
Rais Alpha Condé wa Guinea amesema kuwa,
kuheshimiwa mipaka ya mwaka 1967 ndio njia pekee ya
kuweza kufikiwa
usalama katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Rais Condé
ameyasema hayo katika kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
mjini New York, ambapo pamoja na mambo mengine, amesisitiza juu ya
uungaji mkono wa nchi yake kwa taifa la Palestina na kulaani vikali
jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Ghaza huku akiitaka Tel
Aviv kuheshimu sheria za kimataifa. Vile vile Rais huyo wa Guinea
ameashiria ongezeko la umasikini na uharibifu wa mazingira unaofanywa na
wanadamu na kutaka kuwekwa mikakati madhubuti ya kukabiliana na
matatizo hayo. Aidha ameashiria mgogoro wa afya nchini Sierra Leone,
Liberia na Guinea Conakry na kutaka kukabiliana kwa nguvu zote na janga
hilo ambalo linazidi kushika kasi siku hadi siku katika nchi za
magharibi mwa Afrika. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO),
karibu watu 3,000 wamekwishapoteza maisha tangu mwezi Machi mwaka huu
kulipoibuka ugonjwa huo hatari wa Ebola huko magharibi mwa Afrika.
0 toamaon yako: