Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Friday, September 26

IMF: Dola milioni 130 zimetengwa kuikabili Ebola

Posted by mkachu  |  Tagged as:

IMF: Dola milioni 130 zimetengwa kuikabili EbolaMfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) umetangaza kutengwa kiasi cha dola milioni 130 kwa ajili ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola. Ripoti iliyotolewa na IMF imesisitiza kuwa kiwango hicho cha fedha kitakabidhiwa kwa nchi za magharibi mwa Afrika zikiwemo Guinea Conakry, Liberia na Sierra Leone ambazo zimeathiwa zaidi na ugonjwa huo. Aidha ripoti hiyo imefafanua kuwa msaada huo wa fedha umetengwa kufuatia ombi la nchi hizo juu ya kukabiliana na janga hilo. Siku ya Alkhamisi nchi za Ujerumani, Canada, Marekani, Ufaransa, Italia, Japan na Uingereza ambazo ni wanachama wa kundi la G7, maambukizi ya ugonjwa huo yanapaswa kudhibitiwa kwa njia yoyote ile, lakini zikasisitiza pia juu ya kutotengwa nchi zilizoathiriwa na tatizo hilo. Viongozi wa nchi hizo waliyasema hayo kando na kikao cha 69 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York. Ugonjwa wa Ebola uliibuka mwishoni mwa mwaka jana nchini Guinea Conakry na kuenea kwa haraka katika nchi nyingine jirani kama Liberia, Sierra Leone, Nigeria na Senegal.

 

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com