
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mashambulizi ya anga ya Marekani dhidi ya
kundi la Daesh ni ya kimaonyesho. Rais Rouhani amesema kuwa,
mashambulizi hayo hayawezi kukabiliana wala kuliangamiza kundi hilo
ambalo linahama kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Rais Rouhani alisema
hayo jana katika mahojiano na kanali ya televisheni ya Marekani ya CNN,
na kusisitiza kuwa, mashambulizi ya Marekani dhidi ya kundi hilo, ni
vita vya kisaikolojia na wala si operesheni za kijeshi kama inavyodaiwa
na Washington. Rais Hassan Rouhani amesema, mashambulizi hayo ni hadaa
kwa ulimwengu. Kwengineko Rais Rouhani ameashiria mazungumzo ya nyuklia
kwa kusema kuwa, kufikiwa makubaliano ya muda mfupi, ni ishara kwamba
mazungumzo yamefanikiwa. Amesema kuwa kila upande wa mazungumzo unaamini
kuwa, mazungumzo ndio njia pekee ya utatuzi wa kadhia ya nyuklia na si
vinginevyo. Hii ikiwa na maana kwamba, vikwazo na vitisho ni mambo
yasiyo na nafasi yoyote ile.
0 toamaon yako: