Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen amesema kuwa,
makubaliano ya usitishaji mapigano yamefikiwa kati ya serikali na
wapiganaji wa Houthi. Jamal Bin Omar ameeleza kuwa, makubaliano hayo ni
waraka wa kitaifa utakaoandaa njia ya mabadiliko ya amani, na kuweka
msingi wa ushirikiano wa kitaifa na kuimarishwa amani na usalama.
Ameongeza kuwa, matayarisho yamefanywa kwa ajili ya kufanyika hafla ya
kusainiwa makubaliano hayo ya usitishaji vita hii leo.
Hayo yamejiri baada ya kujiri mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na wapiganaji wa Kishia wa Houth ambao walifanikiwa kuzingira kwa muda makao makuu ya televisheni ya taifa mjini San’aa. Zaidi ya watu 100 wamefariki dunia nchini Yemen toka Alkhamisi kutokana na mapigano hayo.
Wafuasi wa Harakati ya Ansarullah na waungaji mkono wao wamekuwa wakifanya maandamano mjini Sana'a kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa wakitaka serikali mpya iundwe.

0 toamaon yako: