
Raia wa Sierra Leone wamesalia majumbani mwao
kwa siku ya pili mfululizo wakati ambapo taifa hilo linatekeleza agizo
la kutotoka nje la masaa 72 ili kujaribu kusitisha ueneaji wa ugonjwa wa
Ebola.
Mwandishi wetu anasema kuwa kituo cha oparesheni za dharura kilipokea zaidi ya simu 900 katika siku ya kwanza ya agizo hilo,kupitia kuwaripoti wagonjwa ama kutaka miili ya wafu kuchukuliwa.
Amesema kuwa kuna vituo viwili pekee katika taifa hilo na kwamba kituo kimoja katika eneo la Kenema kimejaa wagonjwa.
0 toamaon yako: