
Wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria wameshambulia mji wa kazkazini mashariki wa Mainok karibu na mji wa Maiduguri.
Walioshuhudia wanasema kuwa wapiganaji hao walibeba chakula katika magari ya wizi,huku wanajeshi wakitoroka.
Kundi la Boko haram limechukua udhibiti wa miji kadhaa na vijiji katika mji wa Maiduguri katika majuma ya hivi karibuni.
Jeshi limejaribu kulikabili kundi hilo licha ya tangazo la hali ya hatari katika majimbo mjatatu ya kazkazini mashariki mwa Nigeria mwaka uliopita.
0 toamaon yako: