Raisi wa Marekani Barack Obama amesema Afrika Magharibi inakabiliwa na janga la kibinaadam na kutaka dunia ichukue hatua haraka kuumaliza ugonjwa wa Ebola.
Obama amesema katika kikao cha dharula cha Umoja wa mataifa kuwa kuingilia kati swala hili kutaponya maisha ya maelfu ya watu.
Raisi wa liberia Ellen Johnson Sirleaf ameuambia mkutano huo kuwa ugonjwa wa ebola ulikua adui asiyejulikana aliyegharimu maisha ya watu 1700 wa nchini mwake.
Naye Raisi wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma, ameutaja ugonjwa wa ebola kuwa gonjwa la dunia, akiitaka jumuia ya kimataifa kuchukua hatua.
Benki ya dunia imetangaza kuongeza msaada wa kifedha wa dola milioni mia moja na sabini kusaidia kupambana na ugonjwa huo.
0 toamaon yako: