Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Friday, September 26

Ijumaa, 26 Septemba, 2014

Posted by mkachu  |  Tagged as:


Ijumaa, 26 Septemba, 2014
Leo ni Ijumaa tarehe Mosi Dhulhija 1435 Hijria sawa na Septemba 26, 2014.
Siku kama ya leo miaka 1433 iliyopita, Bibi Fatima binti ya Mtume SAW alianza maisha mapya baada ya kufunga ndoa na Imam Ali bin Abi Talib AS. Bibi Fatima alikuwa mwanamke mwema, mtukufu na kigezo bora cha Waislamu. Masahaba mashuhuri walijitokeza kumposa binti huyo wa Mtume. Hata hivyo, Mtume alikuwa akimjibu kila aliyekwenda kumposa binti yake huyo kwamba, suala la ndoa yake liko mikononi mwa Mwenyezi Mungu. Baada ya kufunga ndoa, watukufu hao walianza maisha yao ya kawaida kabisa yaliyojaa huruma, upendo na masuala ya kiroho na kimaanawi. Familia hiyo imeitunuku dunia shakhsia adhimu na wa kupigiwa mfano kama Imam Hassan, Imam Hussein na Bibi Zainab (as).
Siku kama ya leo miaka 107 iliyopita, inayosadifiana na 26 Septemba 1907, nchi ya New Zealand iliyoko mashariki mwa Australia ilipata uhuru. Visiwa vya New Zealand vilikoloniwa na Uingereza mwaka 1769 na karne ya 19 Miladia, ilishuhudia ukoloni dhidi ya nchi hiyo ukishadidi sambamba na wimbi kubwa la wahajiri wa Kiingereza waliokuwa wakielekea katika nchi hiyo.
Tarehe 26 Septemba mwaka 1962, mfumo wa utawala wa Kifalme katika nchi ya Yemen ya Kaskazini ulifikia tamati. Kiongozi wa nchi hiyo alikuwa akijulikana kwa jina la Imam. Kanali Abdullah Sallal alifanya mapinduzi katika siku kama ya leo na kuhitimisha mfumo wa utawala wa Kifalme katika nchi hiyo na kisha kutangaza mfumo wa utawala wa serikali ya Jamhuri kuwa ndio utakaoingoza nchi hiyo.
Na siku kama ya leo miaka 54 iliyopita, inayosadifiana na 26 Septemba 1960, Makamu wa Rais wa Marekani Richard Nixon na Seneta John F. Kennedy wa Massachusetts walikabiliana katika mdahalo wa kwanza wa televisheni wakati wakiwania tiketi ya kuingia ikulu ya White House. John Kennedy aliibuka na ushindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka huo

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com