Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Tuesday, September 23

Maseneta wa Kenya wakutana na Naibu Waziri wa Iran

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Maseneta wa Kenya wakutana na Naibu Waziri wa IranNaibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, Tehran ina shaka na nia ya Marekani ya kutaka kupambana na ugaidi. Akizungumza na ujumbe wa maseneta kutoka nchini Kenya ulioko nchini, Hussein Amir Abdulahiyan amesema kuwa, mara baada ya kuanza mgogoro wa Syria, Iran ilizitahadharisha nchi za Magharibi juu ya matokeo mabaya na hatari ya kuyaunga mkono  makundi ya kigaidi. Abdulahiyan ameongeza kuwa, baada ya kupita muongo mmoja makundi yanayofungamana na al Qaeda yamekuwa na uzoefu mkubwa katika kutekeleza operesheni zao za kigaidi katika nchi za Afghanistan na Iraq. Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesema kuwa, uhusiano wa Tehran na Nairobi uko katika kiwango kizuri, na kusisitiza kwamba nafasi ya mabunge na hasa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ina nafasi muhimu mno. Kwenye mazungumzo hayo, Muhammad Yussuf Haji, Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni katika Bunge la Seneti la Kenya ameelezea azma ya serikali ya nchi yake ya kuimarisha mashirikiano na Iran na kusisitiza kwamba Nairobi ina taarifa za kutosha kuhusu hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa na Iran katika nyanja za elimu na teknolojia. Haji ameongeza kuwa, Kenya inataka mashirikiano ya pande mbili katika nyanja mbalimbali yaimarishwe zaidi.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com