Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Tuesday, September 23

Ebola yatokomezwa kikamilifu nchini Kongo DR

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Ebola yatokomezwa kikamilifu nchini Kongo DRWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, ugonjwa wa ebola ambao unaendelea kusambaa kwa kasi katika eneo la magharibi mwa Afrika, umeweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa nchini Kongo. Augustin Matata Ponyo amesema kuwa, katika siku za hivi karibuni hakujashuhudiwa kesi yoyote inayohusiana na maradhi ya ebola nchini humo. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo amesema kuwa, idadi ya watu waliopatwa na maradhi hayo kuanzia mwezi uliopita hadi sasa ni 68, na wengine 41 wameshafariki dunia kutokana na ugonjwa huo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani WHO, zaidi ya watu 2,700 wameshafariki dunia hususan katika nchi za Liberia, Guinea na Sierra Leone kutokana na maradhi ya ebola.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com