Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Tuesday, September 23

Maadui wauvunjia heshima Msikiti nchini Ufaransa

Posted by mkachu  |  Tagged as:

http://kiswahili.irib.ir/media/k2/items/cache/d697a0ab0253781e57ca2c39c1013f9a_XL.jpgKundi la watu wenye misimamo ya chuki dhidi ya dini tukufu ya Kiislamu nchini Ufaransa wameuvunjia heshima Msikiti katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo. Gazeti la Le Figaro linalochapishwa nchini Ufaransa limeandika kuwa, mfanyakazi wa msikiti ulioko katika eneo la Pontarlier mashariki mwa Ufaransa, jana aliushuhudia mzoga wa nguruwe uliotupwa kwenye mlango wa kuingilia msikitini. Taasisi kadhaa za Kiislamu nchini Ufaransa zimetoa tamko la kulaani vikali kitendo hicho, kinachokinzana na uhuru wa kuabudu. Polisi ya Ufaransa imeshaanza uchunguzi kuhusiana na kitendo hicho kinachoonyesha wazi kuwepo chuki dhidi ya dini ya Kiislamu nchini humo. Kiongozi wa serikali katika eneo hilo amelaani kitendo hicho na kusisitiza kwamba, serikali ya Paris itaendeleza juhudi za kuwasaka na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria wahusika wote wa kitendo hicho. Naye mmoja kati ya viongozi wa Baraza la Waislamu wa Ufaransa CFCM amesema kuwa, tokea yaliposhadidi machafuko katika eneo la Mashariki ya Kati, vitendo vya chuki na uadui dhidi ya dini ya Kiislamu vimeongezeka, katika hali ambayo Waislamu wanataka kuishi na wafuasi wa dini nyingine nchini humo kwa amani.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com