Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Tuesday, September 23

Keita asisitizia kupatikana maridhiano ya kitaifa Mali

Posted by mkachu  |  Tagged as:

Keita asisitizia kupatikana maridhiano ya kitaifa MaliRais Ibrahim Boubacar Keita wa Mali ametoa wito wa kupatikana maridhiano ya kitaifa katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika inayokabiliwa na mgogoro wa kisiasa na kiusalama. Rais Keita amesisitiza juu ya udharura wa kupatikana maridhiano ya kitaifa katika maeneo yote ya nchi hiyo. Rais wa Mali ameashiria mazungumzo ya amani yanayoendelea huko Algeria kati ya ujumbe wa serikali ya Bamako na wapinzani na kusisitiza kwamba, bila shaka hata hao wanaoshiriki katika mazungumzo hayo wanataka kufikiwa maridhiano ya kitiafa katika nchi yao. Duru ya pili ya mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Mali na makundi yanayobeba silaha ya kaskazini mwa nchi hiyo ilianza tarehe Mosi mwezi huu katika mji mkuu wa Algeria, Algiers. Awamu ya kwanza ya mazungumzo hayo ilifanyika tarehe 4 Julai katika mji huo huo ambapo pande mbili zilitia saini ramani ya njia ya mazungumzo kati yao. Serikali ya Mali imekuwa ikikabiliwa na mgogoro wa kisiasa tangu Januari mwaka 2012 baada ya makundi yenye silaha kuanzisha mashambulio katika maeneo ya kaskazini mwa nchi hiyo.

Related Posts:

0 toamaon yako:

    Author

    CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

    uislam na maisha yake

    uzayuni

    swahili radio

    uislam na maisha

    mohamed waziri

    Subscribe to our Mailing List

    We'll never share your Email address.
    +255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com