
Jitihada zimeendelea kufanywa katika
nchi kadhaa za Afrika magharibi na jumuia ya kimataifa kupambana na
ugonjwa wa ebola ambao umeathiri nchi za Sierra Leone,Liberia , Guinea
hali kadhalika Nigeria kwa kiasi kikubwa huku Serikali za nchi hizo
zikifanya jitihada za kujinusuru na ugonjwa huo.
Baadhi ya shule
Nchini Nigeria zimefunguliwa baada ya kuchelewa kwa zaidi ya wiki mbili
kwa lengo la kujaribu kuzuia maambukizi ya ugonjwa ebola lakini shule
zilizopo mjini lagos ambapo ndio kitovu cha ugonjwa huo zitaendelea
kufungwa mpaka mwezi ujao .
Shirikisho la walimu nchini humo
linaitaka serikali kuchukua hatua ili kuzuia tishio la maambukizi ya
ugonjwa wa ebola kwa wanafunzi, na kusema kuwa wamesitisha mgomo
Wakati
huo huo, Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa maambukizi ya
virusi vya ebola yamedhibitiwa nchini Nigeria na Senegal miongoni mwa
nchi tano ambazo ugonjwa wa ebola umeua karibia watu 2800.
Raia wa
Nchi jirani Sierra Leone walilazimika kujifungia ndani wa mda wa siku
tatu kujinusuru na ebola zoezi ambalo viongozi wamesema kuwa
limefanikiwa.
0 toamaon yako: