Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Tuesday, September 23

Vyombo vya usalama Yemen vimesambaratika

Posted by mkachu  |  Tagged as:

"Vyombo vya usalama Yemen vimesambaratika" 

                            Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen amesema kuwa, vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo vimesambaratika kikamilifu. 

                             Akizungumza mjini Sana'a, Jamal bin Omar amesisitiza kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vya Yemen vimesambaratika na hata katika baadhi ya maeneo ya nchi hiyo hakuna usalama kabisa na maeneo mengine yanadhibitiwa kikamilifu na makundi ya wanamgambo wanaobeba silaha.

                         Wakati huohuo, Wizara ya Afya ya Yemen imetangaza kuwa, kwa akali watu 200 wameuawa na wengine 461 kujeruhiwa baada ya kujiri mapigano hivi karibuni mjini Sana'a kati ya wanaharakati wa al Houthi na wafuasi wa chama cha al Islaah, kinachoungwa mkono na jeshi la nchi hiyo. Taarifa zaidi zinasema kuwa, usalama umeshaanza kurejea tena kwa kiwango fulani nchini Yemen, baada ya kutiwa saini makubaliano ya kisiasa na ya amani kati ya Rais wa Yemen na harakati ya al Houthi.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com