Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Sunday, September 28

Kuendelea maandamano sambamba na ongezeko la fikra za kufurutu ada nchini Saudia

Posted by mkachu  |  Tagged as: ,

Kuendelea maandamano sambamba na ongezeko la fikra za kufurutu ada nchini Saudiaanjari na kuendelea maandamano ya wananchi wanaotaka haki zao za kimsingi, hivi sasa Saudia inakabiliwa pia na ongezeko la fikra za makundi ya kufurutu ada nchini humo. Kuanzia Ijumaa iliyopita eneo la Qatwif, mashariki mwa nchi hiyo, limekuwa likishuhudia maandamano ya wananchi dhidi ya utawala wa kifalme wa nchi hiyo. Katika maandamano hayo, waandamanaji wanasisitizia juu ya kuachiliwa huru wafungwa wa kisiasa na kuhitimishwa ukandamizaji na mashinikizo dhidi ya raia. Hata hivyo duru za habari nchini humo zinaarifu kuwa, katika kujaribu kuzima maandamano hayo, askari wa Aal-Saud wamekuwa wakishambulia Swaandamanaji kwa risasi na mabomu ya kutoa machoni, na kupelekea kujeruhiwa makumi ya waandamanaji huku wengine wakitiwa mbaroni. Aidha askari hao wa Saudia, wamemtia mbaroni Basim al-Qudayhi, kijana aliyejeruhiwa vibaya katika maandamano ya siku za nyuma na ambaye alikuwa bado anaendelea kupata matibabu hospitalini kwa lengo la kuokoa maisha yake. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Saudia sanjari na kuthibitisha kutiwa mbaroni al-Qudayhi, imetangaza kuwa kijana huyo alitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuhusika eti na mashambulizi ya silaha dhidi ya maafisa usalama, kutishia maisha ya raia n a kutoa mafunzo ya kijeshi kwa watoto wadogo wa nchi hiyo, tuhuma ambazo zimetajwa na wapinzani kuwa ni za kubambikiziwa al-Qudayhi na ambazo hadi sasa hazijathibitishwa na pande zozote huru. Hii ni katika hali ambayo wakazi wengi wa mkoa wa al-Sharqiyyah, hapo jana asubuhi pia walifanya maandamano ya amani yaliyoitishwa na Muungano wa Uhuru na Uadilifu chini ya kaulimbiu ya 'Lazima Kuvunjwa Mzingiro', maandamano ambayo pia yalikabiliwa na hujuma ya askari usalama wa Saudia. Hapo jana mtandao wa habari wa al-Ahd wa Saudia pia uliandika kuwa, kuanzia asubuhi ya jana Jumamosi, mji wa Qatwif ulizingirwa kikamilifu na askari wa utawala wa Aal-Saud sanjari na kuwekwa vituo vya ukaguzi vya kutoka na kuingia katika mji huo. Mbali na hayo, nchini Saudia kumeripotiwa habari za ongezeko la fikra za kufurutu ada za Kidaesh katika maeneo tofauti ya nchi hiyo suala ambalo linatajwa kuwatia khofu watawala wa Riyadh. Kuhusu hilo, maandishi yafautayo, "Daesh imo katika mioyo yetu," yalipatikana yameandikwa katika moja ya milango ya shule za wasichana iliyoko katika mji wa Al Khurma, kaskazini mashariki mwa mkoa wa Taif, maandishi ambayo yamewaogofya sana viongozi wa Saudia. Kwa mujibu wa duru za habari, maafisa usalama katika mkoa huo wameanzisha upelelezi wa kugundua mwandishi wa maneno hayo. Inaelezwa kuwa, uharibifu wa mali za umma na kadhalika kuenea kwa fikra za kufurutu ada, ni sababu mbili muhimu zilizopelekea viongozi wa Saudia kuanzisha uchunguzi wa mwandishi wa maneno hayo. Ni vyema kufahamika hapa kuwa, wasiwasi wa viongozi wa utawala wa kifalme nchini Saudia juu ya ongezeko la fikra za kufurutu ada hususan fikra za Kidaesh, unakuja katika hali ambayo kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni Saudia imekuwa moja ya waungaji mkono wakuu wa makundi ya kigaidi likiwemo kundi hili la kitakfiri na kigaidi linalojiita eti Dola la Kiislamu nchini Iraq na Sham 'Daesh'. Hivi sasa sanjari na utawala huo kufanya njama za kuzima au kupunguza wimbi la maandamano dhidi yake, unapaswa pia kukabiliana au kupunguza fikra za kitakfiri na tishio la makundi ya kigaidi hususan lile la Daesh nchini humo.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com