
Kundi la wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya
Misri leo Jumapili limefanya maandamano katika meidani ya Tahrir
wakipinga safari ya leo alasiri ya Rais Abdul Fatah al Sisi wa nchi hiyo
katika Chuo Kikuu cha Cairo. Makumi ya wanachuo ambao ni wanachama wa
Harakati ya Wanachuo wanaopinga mapinduzi ya kijeshi wameshiriki kwenye
maandamano hayo katika meidani ya Tahrir huko Cairo na kupiga nara dhidi
ya Rais wa Misri na utawala ulioko madarakani. Wanachuo hao wametangaza
kuwa hii ni hatua yao ya kwanza katika kupinga safari ya Rais wa Misri
katika Chuo Kikuu cha Cairo. Hii ni katika hali ambayo, mw
aka jana Vyuo
Vikuu vya nchini Misri karibu kila siku vilikuwa vikishuhudia maandamano
makubwa ya wanachuo wafuasi wa Mohamed Morsi Rais wa zamani wa nchi
hiyo aliyepinduliwa na jeshi, maandamano ambayo wakati mwingine yalikuwa
yakisababisha ghasia na machafuko na kupelekea wanachuo kadhaa kuuawa
na kujeruhiwa na makumi ya wengine kutiwa nguvuni. Aidha wanafunzi
wengine wa Vyuo Vikuu nchini Misri walifukuzwa chuo kutokana na
kushiriki kwao katika maandamano.
0 toamaon yako: