
Algeria imesema kuwa imechukua umauzi wa
kujenga ukuta wa usalama wenye urefu wa kilomita 110 katika mipaka ya
nchi hiyo na Libya. Algeria imeamua kujenga ukuta huo wa umeme baada ya
kufanya mazungumzo na maafisa usalama na kwa kuwasiliana na Libya,
katika kikao kilichowashirikisha pia wataalamu wa masuala ya kupambana
na ugaidi na jinai zilizoratibiwa. Algeria imesema kuwa vikosi vya
usalama vitatumwa kwenye mipaka ya pamoja ya nchi mbili hizo, sambamba
na kujengwa ukuta huo wa umeme.
0 toamaon yako: