
Ibrahim al Ja'afari Waziri wa Mambo ya
Nje wa Iraq kwa mara nyingine ametahadharisha kuhusu tishio kuu la
magaidi wa kitakfiri wa Daesh na kukanusha kuweko vikosi vya kigeni vya
nchi kavu huko Iraq kwa ajili ya kukabiliana na kundi hilo la kigaidi.
Mwanadiplomasia huyo wa ngazi ya juu wa Iraq amesisitiza kuwa serikali
ya Baghdad haijawahi kuomba msaada wa vikosi vya nchi kavu kutoka nje
kwa ajili ya kupambana na Daesh. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iraq
ameyasema hayo pambizoni mwa mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa
Mataifa mjini New York Marekani katika mazungumzo yake na Walid al
Muallim Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria na mawaziri wenzake wa Uchina,
Japan na Korea Kusini.
Ibrahim Ja'aafari ametilia mkazo kwamba, msaada
wa kutosha wa mashambulizi ya anga yanalisaidia jeshi la Iraq na vikosi
vya kujitolea vya wananchi pamoja na wapiganaji wa Kikurdi wa Peshmerga
kupambana na magaidi wa kitakfiri wa Daesh hivyo Iraq haihitajii vikosi
vya kigeni vya nchi kavu katika kupambana na kundi hilo.
0 toamaon yako: