Tanzania swahili radio

IQRA FM RADIO

IQRA FM RADIO
IQRA FM RADIO ELIMU NA MATENDO UIMARA WA RADIO IQRA UPO MIKONOMI MWAKO CHANGIA RADIO IQRA KWA MPESA 0762118805TIGO PESA 0658118804

Wednesday, September 24

Bilioni 2.3 kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

Posted by mkachu  |  Tagged as:


Bilioni 2.3 kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
Viongozi wa dunia wameahidi dola bilioni 2.3 katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, kwa lengo la kusaidia maendeleo ya nchi katika kukabiliana na madhara yanayotokana na ongezeko la joto la dunia.  Mwishoni mwa kikao hicho Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ametoa wito wa kufanywa jitihada za kufikiwa makubaliano ya dunia ya tabianchi ifikapo mwaka kesho, na kuwataka viongozi wa dunia watekeleze majukumu yao katika kulinda sayari ya dunia kwa kupunguza joto la dunia kwa  nyuzi joto 2.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa pia ametaka viongozi wa dunia wachukue hatua zaidi za kupunguza gesi za nyumba ya kioo, kuzuia kukatwa misitu na kusaidia nchi masikini kukabiliana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa kama vile ukame, mafuriko, vimbunga na kupanda kiwango cha maji ya bahari.
Kwa muda mrefu sasa nchi zinazoendelea zimekuwa zikitaka kusaiiniwe makubaliano kuhusu tabianchi bila kujali ahadi za Marekani, zikisema kuwa nchi hiyo tajiri na iliyoendelea ndiyo inayochangia pakubwa katika kuharibu hali ya hewa duniani.

0 toamaon yako:

Author

CONTACT ME FOR WEB AND BLOG DESIGNING...

uislam na maisha yake

uzayuni

swahili radio

uislam na maisha

mohamed waziri

Subscribe to our Mailing List

We'll never share your Email address.
+255 (762) 118-805 mohamedwaziri295@gmail.com